Menstrual pad with red glitter on blue colored background

Sababu nane za kuchelewa kwa kunyesha

Unawasiwasi kwa kuwa umechelewa kunyesha alaa?. Usianze kuwekeza katika kununua vipande vya nguo, kukosa kunyesha au kuchelewa kunyesha kunasababishwa na sababu nyingi sana mbali na mimba.

Kuna nyakati mbili hasa katika maisha ya wanawake ambayo ni kawaida tu sana kwa kunyesha kubadilika ghafla.

Wakati ambao inaanza na wakati mwanamke anapoanza usee.

Kwa mamama wengi mvua yao huja baada ya siku 28. Kwa wengine mfumo wa kawaida na wa kiafya unaeza tokea kila siku 21 hadi 35.

Mara nyingine kunyesha pia inaezachelewa na dalili zinaeza kuwa boli. Pia kuna sababu mob sana za kusababisha kuchelewa kunyesha kwa mamama.

Mvua yako pia inaeza kuchelewa kutokana na sababu zifuatazo

1. Msongo wa mawazo

Stress tu kiasi haziezi umiza lakini stress mob zitakukoroga. Stress za muda au stress kibao zinaeza athiri homoni zako zinazodhibiti mayai hali inayochangia kuchelewa au kokosa mvua yako. Lakini msee ni poa kukumbuka kuwa kile unachofikiria kinakutia stress mwingine ako tu poa namaanisha haimtii mwingine stress.

2. Kukata weight

Umekata weight sana au umeongeza weight. Unapokata weight au kuongeza weight unaeza athiri mfumo wako wa kunyesha. Shida za kiafya hasa kukosa kula kwa kukosa hamu au kula kupita kiasi pia zimesemakana kusababisha kuchelewa kunyesha.

Msee mafuta mengi mwilini pia huathiri kiwango cha homoni za hisia ambayo mwili wako hutoa na kiwango kikubwa au kichache cha homoni za hisia zinaweza pia kuathiri hali yako ya kutoa mayai na kunyesha.

3. Matumizi ya kinga

 Msee unapoenda kinyume na mfumo mzima wa kupanga uzazi unaeza kupata mabadiliko ya mfumo wako wa kunyesha. Hizi njia za kupanga uzazi zina homoni ambazo huathiri afya ya uzazi na huzuia mifuko ya mayai kutoa mayai. Pia hii inaeza tokea ka utatumia vdawa za kupanga uzazi zakueka kwenye ngozi, zakumeza au zakujidunga/kujibwenga.

4. Michezo kupita kiwango

Mazoezi mengi kuzidisha pia yanaeza sababisha kukosa mvua yako ya mwezi au hata uikose. Mazoezi zaidi yanaeza punguza kiwango chako cha homoni ya hisia ambayo hudhibiti system yako ya kizazi. Wachezaji wengine pia wanaweza kosa kunyesha kwa miezi sita au hata zaidi kutokana na mazoezi mob.

5) Matibabu

Baadhi ya matibabu pia yanaeza kuathiri mfumo wako wa kunyesha. Iwapo unatumia dawa inawezekana mojawapo ya athari ni mvua ambayo inayumbayumba. Hii pia unajua ni miongoni mwa utumizi wa dawa fulani za kupanga uzazi

6) Magonjwa

Baadhi ya magonjwa pia yanasababisha kuchelewa kwa hali yako ya kunyesha. Hii ni kweli kutokana na magonjwa ambayo yamefikia kiwango hatari kama vile sukari na uvimbe kwenye ubongo na ugonjwa  unaoathiri utumbo mdogo . Magonjwa haya yanaeza athiri hali yako ya kike mara mob. Kwa mfano sukari ambayo huezi kuimanage inaweza kusababisha kuchelewesha kunyesha kwa madem kutokana na mabadiliko katika kiwango cha sukari.

Ugonjwa unaosabisha uvimbe au kufura fura kwa mfuko wa mayai husababisha viwango tofauti vya homoni ambayo pia husababisha kunyesha kuchelewe au kukawie.  Wanawake wanaougua ugonjwa huu wanaweza kutoa homoni nyingi ya androgen(Homoni yakiume) ambayo inaeza kuonekana wazi kwa mutu mwenye manywele mob mwilini au kwenye uso.

7) kipindi cha kabla ya kukoma wa hedhi

Iwapo unakaribia miaka hamsini unaeza kupata mvua yako kuchelewa kutokana na hali hali ya uzee unaokukodolea macho.

Kuchelewa kwa hedhi zako kunatokana na kupungua kwa homoni ya oestrogen. Mara nyingine wanawake waliochini ya umri wa miaka 45 wanaeza kucheleweshwa au hata kukosa hedhi zao kutokana na kukoma kwa hedhi mapema kunakoletwa na uzee .

8) Kusafiri

Kusafiri kwa mwendo mrefu pia kunaeza kuathiri mwili wako kukasababisha kuathiri hali yako ya hedhi .Kunaweza pia sababisha hedhi zako kuja mapema au kuchelewa. Au hata ukose kabisa.

Daktari wako anaeza kukupima na kujua sababu za kukosa kunyesha kwako na hata akupe matibabu. Ni muhimu hata hivyo kuweka rekodi ya mfumo wako wa kunyesha kila mwezi ili kuonyesha daktari wako.

Pia mtembela daktari wako ili akucheki poa.

did you find this useful?

Tell us what you think

Recent Comments (2)

  1. What should a widow or a widower do to keep sexual health?

    1. The best thing to do is to educate yourself about sexual health and always seek medical attention and go for tests as recommended by your doctor. We are happy to be your choice for information on sexual health so feel free to engage with us here or on social media.

      Cheers!

LoveMatters Africa

Blush-free facts and stories about love, sex, and relationships